EYA imeendelea kusimama bega kwa bega na wasichana wenye umri wa miaka 14–25 kwa kuwapa elimu kuhusu matumizi sahihi ya taulo za kike na umuhimu wa usafi wa hedhi.
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa hakuna msichana anayekosa furaha, kujiamini, au kukatisha masomo yake kwa sababu ya hedhi. Kupitia elimu, mazungumzo ya wazi, na ugawaji wa taulo za kike, tumewasaidia wasichana hawa kuelewa miili yao, kujitunza kwa usahihi, na kuondoa aibu au hofu inayoweza kuathiri maisha yao ya kila siku.
Hedhi si kikwazo cha ndoto. Ni sehemu ya maisha ya kawaida ya mwanamke. Tunataka kila msichana aendelee na masomo yake, ahudhurie shule kwa ujasiri, na kuishi kwa furaha hata akiwa katika siku zake.
Kupitia hatua hii ndogo ya upendo na elimu, tunaamini tunachangia kujenga kizazi chenye afya, kujiamini na chenye uwezo wa kufikia ndoto zao.
Be Different, Be Brave, Be You! 🌿

