10th march Women judge day

Katika kuadhimisha Siku ya Majaji Wanawake Duniani, sisi EYA tunatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wanawake majaji katika kusimamia haki, usawa na utawala wa sheria katika jamii.
Wanawake katika mfumo wa mahakama wanaendelea kuwa sauti muhimu katika kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wote bila ubaguzi. Uongozi wao unaimarisha imani ya jamii katika mfumo wa sheria na kusaidia kujenga jamii yenye usawa na haki.
Uongozi wa Wanawake katika Mahakama, Haki Inaimarika.
EYA tunaendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha usawa wa kijinsia katika sekta ya sheria na kuhamasisha wanawake na wasichana wengi zaidi kufuata taaluma za sheria na uongozi.
EYA – Pamoja dhidi ya ubaguzi, kwa usawa na haki kwa wote.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSwahili